Rais Samia apokea Ripoti ya CAG na Taarifa ya Utendaji kazi ya TAKUKURU 2022/2023

By Frank Monyo , Nipashe
Published at 06:27 PM Mar 28 2024
Picha ya kusanifiwa ya Rais Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba baada ya kupokea Ripoti ya CAG na Taarifa ya Utendaji kazi ya TAKUKURU 2022/2023 (Kushoto juu) Mkurugenzi TAKUKURU CP Salum Rashid Hamduni, chini CAG Charles Kichere.
Picha: Nipashe Digital, IKULU
Picha ya kusanifiwa ya Rais Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba baada ya kupokea Ripoti ya CAG na Taarifa ya Utendaji kazi ya TAKUKURU 2022/2023 (Kushoto juu) Mkurugenzi TAKUKURU CP Salum Rashid Hamduni, chini CAG Charles Kichere.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2022/2023 pamoja na taarifa ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2022/2023 leo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 28 Machi, 2024.

Akiwasilisha Taarifa ya Utendaji kazi wa TAKUKURU, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, CP Salum Rashid Hamduni, amesema taasisi hiyo katika operesheni mbalimbali za kiuchunguzi imefanikiwa kuokoa bilioni 87.59 na uokoaji huo ulihusisha uokoaji wa dola za kimarekani milioni 33 sawa na shilingi bilioni 36.34

Kupitia uchunguzi wa mkongo wa taifa ambao ulibainika kuwa Umoja wa Watoa Huduma za Mawasiliono ulijenga miundombinu ya mawasiliano kinyeme na makubaliano na hivyo kuikosesha serikali mapato kutokana na huduma zao kutopita katika mkongo wa taifa.